MBWA MWITU ALIYEMYONYESHA NA KUMTUNZA MFALME WA RUMI (ROMA)


   
Palikuwa na mji mmojawapo wa Kilatini ambao mfalme wake aliamuru kuwatupa mtoni Tibrisi watoto pacha wa kiume, Romulus na Remus wakiwa ndio kwanza tu wamezaliwa na binamu yake mfalme huyo kwani aliogopa kupokonywa utawala wake watakapokuwa. Kwa wakati huo mto Tibrisi ulikuwa umefurika na susu lilitupwa majini likiwa na watoto hao ndani yake. Kwa bahati nzuri susu hilo lilikwama kwenye tawi la mti ulioanguka na kuelea mtoni.Watoto hao wakanusurika,wakaokotwa na mbwa jike wa mwituni, akawanyonyesha maziwa yake ili wasife njaa. Halafu baadaye wakagunduliwa na mchungaji ambaye aliwatunza mpaka wakakua na kuwa maaskari wenye nguvu na ushujaa mwingi.Wakazusha uasi dhidi ya mfalme yule wakamwua kisha ndugu hao, Romulus na Remus wakaamua kujenga mji ila tu waligombana juu ya mahali pa kuujenga na nani atakayekuja kuutawala. Ugomvi ukazidi na  ukapelekea Romulus akamwua Remus. Karibu na pale yeye na nduguye walipogunduliwa na mchungaji, Romulus akajenga mji,na huo ukawa ndio Rumi au kwa kilatini-Roma.

Vyanzo vya kihistoria vinasema mji wa huo ulichomoza mnamo 753 B.C  na tangu hapo ndipo walipooanza hesabu za miaka ya historia yao. Baadaye kwenye kilima cha kapitoli (capital) huko Rumi kilijengwa sanamu la mbwa jike yule aliyewaokoa Romulus na Remus. Sanamu hiyo kwa sasa linahifadhiwa kwenye makumbusho.

Habari kwa msaada wa Mr. Boniphace Keraryo.

Important: You are allowed to re-post this article on your website or blog as long as you acknoweledge the original author and give the backlink to this site.

Geofrey Mtatiro

I'm a storyteller by trade but a problem-solver by birth. I find creative ways to tell stories of Individuals, Brands, Businesses & Organizations through Photography, Film Production & Advertising. In 2012, I founded BRAINBONGO to do just that while still in high school with the help of a few friends. Through the years, we have become really good at it. We love it and we live it. We are #EXTRAORDINARY!

Post a Comment

If you like this post be sure to leave a comment and share it with your friends. It will make my day!

Previous Post Next Post

Contact Form